Jumanne, 29 Agosti 2017

SALA KWA WANAFUNZI

Shalooom Mpendwa katika Bwana.
Karibu tena katika Blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP.

SALA KWA WANAFUNZI.

Ni Asubuhi nyingine yenye kujaa Utukufu, Eh Mungu wangu, wewe ndiye mkuu wa wakuu, mfalme wa wafalme, usiyeshindwa na jambo, uketie patakatifu pa patakatifu.

Nashkuru kwakua umenilinda mpaka kufikia mahali hapa nilipo, kwamaana si kwa akili zangu wala nguvu zangu, ila ni kwauwezo wako, baraka zako na upendo wako kwangu, na kwa kila neema uliyonijalia, vinanipa ushindi kila siku ya maisha yangu.

Tazama. Nakuja mbele zako eh Mungu wangu,

 Neno lako lasema
"usiiache elimu ikaenda zake kwa maana ndio uzima wangu. "(Mithali 4:13)
Nami hakika sitaiacha elimu, tazama nami napendezwa na kuyatenda mapenzi yako, kwakuwa nalitimiza hilo.

Pia neno lako lasema
" utanifanya kua kichwa na wala si mkia, nami nitakua juu tu, sitakua chini" (Kumb. la Torati 28:13)
kwakuyatimiza mapenzi yako kwa kuwa sijaiacha elimu, hayo yote hayanabudi kutokea katika maisha yangu, kwakua nitakua kichwa na wala si mkia katika maisha ya elimu yangu.

kupitia hayo, nami nitaishi maisha ya ushindi ya kielimu.

Eh Mungu wangu nakupenda kuliko kituchochote, nitakutukuza na kukuabudu wewe tu, siku zote za maisha yangu.

@servant of Jesus
@Henry Sebastian Kibanga
http://upendoworship.blogspot.co.id/?m=1

Jumamosi, 26 Agosti 2017

SALA ZITAKAZO KUKOMBOA KATIKA VIFUNGO VYA MWOVU SHETANI

SHALOOM. Mpendwa katika BWANA
Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP
Tukapate kujifunza sala mbali mbali za kutukomboa kutoka katika vifungo vya yule mwovu shetani

Ningependa kukumbusha kitu kabla ya kujifunza sala hizi
kumbuka ya kuwa BILA KUWA NA IMANI KATIKA MUNGU, HAKUNA UTAKACHO FANIKISHA.

SALA YA KUIKOMBOA MIGUU KUTOKA KWENYE VIFUNGO VYA SHETANI

“Basi, haya ndiyo asemayo Bwana MUNGU;

Atakuwako adui, kuizunguka nchi pande zote; naye atazishusha chini nguvu zako zikutoke; na majumba yako yatatekwa nyara. Haya ndiyo asemayo BWANA; Kama vile mchungaji apokonyavyo kinywani mwa simba miguu miwili, au kipande cha sikio; ndivyo watakavyopokonywa wana wa Israeli, wakaao Samaria katika pembe ya semadari, na juu ya mito ya hariri ya kitanda” (Amosi 3:11—12).

Maandiko yanatuambia tunapambana na falme na mamlaka na Shetani akitaka kupambana kwa kiwango cha kifalme eneo analolenga ni miguu. Mungu naye akitaka kukuokoa ili uujenge ufalme wake analenga miguu. Kuna mahusiano makubwa kati ya agano la damu ya Yesu na miguu. Hivyo tunatumia damu ya Yesu ili kuikomboa miguu katika ulimwengu wa roho:

Fanya sala hii kwa imani ili Mungu aikomboe miguu yako kutoka kwa adui:
🏽

MWENYEZI MUNGU BABA WA MBINGUNI. ASANTE KWA AJILI DAMU YA YESU ILIYOMWAGIKA KWA AJILI YA UKOMBOZI WANGU. KWA MAMLAKA ULIYONIPA KATIKA DAMU YA YESU KRISTO NINAIKOMBOA MIGUU YANGU KUTOKA KWA ADUI. NINAFUTA MANENO YOTE NA HATI YA MASHITAKA YA SHETANI ALIYOPITISHA KWEMYE MIGUU KWA DAMU YA YESU KRISTO. NINAUYEYUSHA UZITO AMBAO SHETANI AMEUWEKA NATIKA NAFSI YANGU KUPITIA MIGUU KWA DAMU YA YESU KRISTO. NINAONDOA UHALALI WA NGUVU ZOTE ZA GIZA ZOTE ZILIZOPITA KWENYE MIGUU NA NINAFUTA JINA LANGU (AU JINA LA…MTAJE MTU) KUTOKA KATIKA MAAGANO YA URITHI KWA DAMU YA YESU KRISTO. MAGONJWA YOTE YALIYOPITA KATIKA MIGUU SASA NAYAMURU YATOKE KATIKA MWILI WANGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO AMEN!!

MSHUKURU MUNGU!


Fanya sala ifuatayo kwa imani ili uikomboe ardhi kwa damu ya Yesu Kristo. Hakikisha unakuwa unatembea kwenye mipaka ya nyumba yako wakati unafanya sala hii:🏽

MWENYEZI MUNGU BABA WA MBINGUNI. ASANTE KWA SABABU UNALITIMIZA NENO LAKO. UMENIAMBIA KUWA MAHALI NITAPOKANYAGA UNANIPA KUMILIKI (Joshua 1:3; Kumbukumbu 11:24—25). NINAMWAGA DAMU YA YESU KRISTO KATIKA ARDHI HII KWA AJILI YA KUONDOA UFALME WA GIZA NA KUWEKA UFALME WA MUNGU (Waebrania 9:22 &Waebrania 10:9) ILI ENEO HILI LITUMIKE KWA AJILI YA KUSUDI LAKO. NGUVU ZOTE ZA GIZA AMBAZO ZINATAWALA ENEO HILI, KWA MAMLAKA NILIYONAYO KATIKA DAMU YA YESU NAZIAMURU ZITOKE. NINAFUTA LAANA ILIYOPO KATIKA ARDHI HII KWA DAMU YA YESU; NINAFUTA KILA UOVU ULIOPATILIZWA  KILA KIZAZI, KIZAZI CHA TATU MPAKA CHA NNE, KWA DAMU YA YESU; NINAFUTA MANENO YOTE YALIYOANDIKWA KWENYE ARDHI ILI NISIFANIKIWE (Yeremiah 22:29—30) KWA DAMU YA YESU KRISTO. NINAFUKUZA KILA WALINZI WA ARDHI KUTOKA KWA ADUI NA NINAAMURU MAPEPO YA ARDHI HII YATOKE KATIKA ARDHI HII KWA DAMU YA YESU. NINATANGUA MAAGANO YALIYOFUNGWA KWENYE HII ARDHI NA NINATENGANISHA KILA MADHABAHU NA VITI VYA ENZI VINAVYOTAWALA KATIKA ARDHI HII KWA DAMU YA YESU KRISTO. NINATOA HUKUMU YA HAKI KWA MIUNGU INAYOTAWALA ARDHI. NINANYUNYIZA DAMU YA YESU NA KUACHAILIA ULINZI WA MBINGUNI KATIKA ARDHI HII KWA JINA LA YESU KRISTO. NAIWEKA WAKFU ARDHI HII ILI MUNGU UUTUMIE KUTIMIZA KUSUDI LAKO KATIKA JINA LA YESU KRISTO AMEN!!

MSHUKURU MUNGU!


Kama umefanya sala hii kwa imani, kama kuna kitu chochote kile Shetani alipitisha kwenye miguu kitaondoka. Kama ulikuwa unapata shida kusoma biblia au kuomba utashangaa wepesi unaoupata.

Ubarikiwe sana Mpendwa Katika BWANA


Jumapili, 20 Agosti 2017

UADUI KATI YA MWANAMKE NA SHETANI.1

SHALOOM Mpendwa katika BWANA.

Karibu tena katika kujifunza neno la Mungu katika blog yako pendwa UpendoWorship


Leo tunaenda kujifunza juu ya uadui uliopo kati ya mwanamke na mwovu shetani.

Labda nianze na kukuuliza swali ambalo nilikua najiuliza hapo kabla, kwanini katika mikutano ya injili, semina mbalimbali za maombezi, na makanisani pia, idadi kubwa sana ya watu wanaosumbuliwa na shetani (mapepo) ni wanawake. Sio kwamba wanaume hawasumbuliwi na mapepo, lakini hapa naangalia idadi kubwa ambayo ni wanawake.
Je! Ulishawahi jiuliza ni kwanini? Bila shaka kwa akili za kibinadamu ni vigumu kutambua hilo, lakini bila shaka, kwa kile chochote kinachoendelea duniani hakika kilishawahi kuandikwa kwenye biblia. Je! maandiko yanasema nini juu ya hili

Ukisoma kwenye kitabu cha biblia Mwanzo 3:13-15 inasema

Mwanzo 3:13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.
Mwanzo 3:14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;
Mwanzo 3:15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. 

Nyoka anayezungumziwa hapo ni shetani, hivyo basi ukiangalia mstari wa 15 apo ndipo utaona kabisa ya kwamba Mungu aliweka uadui kati ya mwanamke na yule nyoka(shetani). Hivyo basi kwa uzao wa mwanamke atamponda kichwa nyoka, naye nyoka atakuponda kisigino ewe mwanamke. Tufaham ya kuwa uzao wa mwanamke ni wale watoto ambao atakuja kuzaa (mimI na wewe tu uzao wa mwanamke) na uzao wa shetani ni mapepo.

Mpaka kufikia hapo nafkiri ushaanza kupata picha halisi ya kua uadui huu umeanzia wapi, na ni kwanini idadi kubwa wanaoteswa na shetani(mapepo) ni wanawake, hii yote ni kwasabu Mungu alishaweka uadui kati yao. Unaweza ukawa unajiuliza kwanini aliweka uadui. Jibu ni kwamba

Ukisoma Biblia kitabu cha Mwanzo 1:1-6, Hapo ndipo utaona ya kua kwanini Mungu alieka uadui kati ya hawa wawili, kwa maana nyoka alimdanganya mwanamke, akala lile tunda kwa kumwambia hatakufa bali atajua mema na mabaya angali walikatazwa na Mungu wasije kula tunda la mti huo.
Mungu alichukizwa na hiko kitendo kiasi akaweka uadui kati yao.

Baada ya kulifahamu hilo, chimbuko la uadui huo twende moja kwa moja katika biblia kitabu cha Ufunuo 12:1-11 na kuendelea mpaka mstari wa 17 ( Ufunuo 12:1-17)

Ni shauku ya moyo wangu upate kusoma hapo li upate maana halisi ya uadui huo na jinsi ulivyokua ukiendelea.

Ukisoma hapo utapata kuona kuna ishara kuu iliyoonekana kutoka Mbinguni, Mwanamke mwenye mimba akilia kwa utungu na kuumwa katika kuzaa, ikaonekana ishara nyingine na tazama joka kubwa(shetani) na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni( nyota hizo ni mapepo) na kuziangusha katika nchi, pia na yule joka akasimama kwa yule mwanamke ili azaapo amle yule mtoto wake. Naye yule mwanamke akazaa mtoto mwanamume naye atakayechunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu na kiti cha enzi. Je mtoto huyo ni nani? Jibu ni Yesu Kristo. Hapo ndipo likatimia lile andiko lisemalo kwa uzao wako ewe mwanamke utamponda kichwa nyoka(shetani). Yesu alimponda kichwa shetani pale msalabani.

Ukisoma Ufunuo 12:15 utazidi kuona ule uadui jinsi unavyozidi, kwa maana nyoka akazidi kupambana na mwanamke, nyoka akatoa katika kinywa chake nyuma ya huyo mwanamke maji kama mto, ili amfanye kuchukuliwa na mto huo yule mwanamke, mstari wa 16 unatuambia Nchi(ardhi) ikamsaidia mwanamke, Nchi ikaifunika kinywa chake,ikaumeza mto ule alioutoa yule nyoka.

(Nyoka anapambana na mwanamke lakini pia nchi"ardhi" inamsaidia mwanamke na ndomana moja ya vita kuu ya kiroho ipo kwenye ardhi, kwasababu pia ardhi ilimsaidia mwanamke)

mstari wa 17, chuki ikazidi kwa maana yule nyoka(shetani) akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake akafanye vita juu ya wazao wake waliosalia(wazao wake hao ni mimi na wewe) wazishikao amri za Mungu, na kua na ushuhuda wa Yesu.....

Natumaini mpaka kufikia hapo ushapata picha halisi kwanini shetani anapambana sana na mwanamke kwa njia mbalimbali iwe kuharibu mimba,kumpandikizia magonjwa,mapepo,mateso, kumfanya mwanamke kutojitambua na kuishi maisha ya kianasa kama ilivyo hivi sasa,hii yote kwasababu ya ule uadui kwa maana shetani anapiagana na hii vita ili kuwinda kile kilichopo ndani ya mwanamke ili kisije kumponda kichwa. Naye shetani akisha kufanikisha kwa kuharibu kwa mwanamke apo tunasema nyoka amekuponda kisigino.

Yesu alipokuja alipitia kwa mwanamke(kwa uweza wa Roho mtakatifu). Likatimia neno, kwa uzao wa mwanamke shetani atapondwa kichwa.

Ewe mwanamke kumbuka vita hii si juu ya damu na nyama bali ni vita ya kiroho, hivyo tambua Mungu ameweka kitu cha pekee kabisa kupitia kwako, hivyo usiishi kizembe zembe, kila mara kumbuka kuombea uzao wako,ombea familia yako ijayo(kama bado huna mtoto), kila mara ombea ardhi,ombea akili yako isije kamatwa na mwovu,ombea fahamu zako, usihishi kibahati mbaya, wewe ni mtu wa tofauti kabisa,usikubali nyoka(shetani) akuponde kwenye kisigino,ombea watoto wako, usiruhu mateso ya kimapepo(uzao wa shetani) yakutese maishni mwako,ombea kila kitu kinachoitwa kwa jina lako, (naposema ombea kila kitu kinachoitwa kwa jina lako namaanisha hata mchumba uliye naye au maraiki au mumeo kwa maana shetani pia anaweza akawatumia hao hao kuja kukuharibia uzao wako)

 Kumbuka tunaye Yesu muweza wa yote, hakuna ashindwalo, kwake yeye utapata kumponda kichwa shetani kama yeye alivyomponda pale msalabani.

usisahau ku share ili pia na wenzako wapate kushiriki baraka za ibada hii
@Henry Sebastian Kibanga.
Instagram@UPENDO WORSHIP

Alhamisi, 17 Agosti 2017

UPENDO WENYE KUZIPONYA NAFSI ZETU

JIFUNZE KUWA NA UPENDO WA KIMUNGU.

Yawezekana kabisa ukawa unafahamu nini maana ya upendo. Labda kwa kusema hivi,
Upendo ni jinsi vile mtu apendavyo iwe kihisia au kutamania au kuweka kitu au jambo kuwa kipaombele ndio kupenda. Wengine husema upendo ni ile hali ya kuwa na amani moyoni juu ya kitu fulani.
Inawezekana ikawa ivyo lakini ni kwa njia ya kila mtu na kwa jinsi alivyopokea neno upendo.
lakini kuna vyanzo vingi sana vya upendo, nazungumzia vitu ambavyo vinamfanya mtu kupelekea kupenda.

Kuna upendo wa kumpenda mtu kwa sababu ya kitu fulani alicho nacho kwa dhumuni la kusaidiwa au kutimiza haja zako.

Kuna upendo wa kindugu, huu ni ule upendo mtu anampenda nduguye, yupo radhi kwenda kulala nae kitanda kimoja hospitali kwa ajili ya kumuhudumia. ( chanzo ni ndugu, lakini asingekua ndugu yake au rafiki yake asingempenda)

Kuna upendo huwa unaibuka kwasababu tu jinsi mtu anaevyoendesha shughuli zake za kimaisha kutokea kupenda vitu kadha wa kadha. (vyanzo maranyingi huwa ni tamaa,ushawishi nk.)

Ukiangalia kwa makini kuna jinsi nyingi sana watu hupelekea kuwa na upendo juu ya kitu au mtu fulani katika maisha yao. Pia inafikia mahala uo upendo walio nao waweza kupelekea kuharibikiwa kimaisha kwa sababu mbali mbali.
Je ni kwanini upendo huo hupelekea kuharibikiwa au kupata matatizo katika maisha yao. Naweza sema ni kwasababu unakua si upendo ambao Mungu wetu mkuu ametuagiza tuwe nao katika maisha yetu.
Mfano upendo ambao Mungu hajaagiza ni kumpenda mtu kwasababu ya kitu fulani, hii itakupelekea kumtegemea mtu huyo kwa ajili ya shida zako. Na pindi unapomtegemea mtu kumbuka Mungu alisema nini katika kitabu cha Yeremia 17:5.

Je Upendo wa Kweli Ni upi ? Upendo aliotuagiza Mungu tuwe nao ni upi ? Au Mungu wetu ana upendo upi ? ili tuufate upendo wa Mungu wetu.

Ukisoma Yohana 3:16 utapata kuuona upendo ambao Mungu wetu anao.
Upendo wa Agape . Huu ni upendo ambao Mungu ametuagiza (anapenda) tuwe nao, ni ule upendo wa hali ya juu sana, ni upendo ambao Mungu wetu mwenyewe anao,upendo ambao haujivuni, upendo ambao hautampenda mtu tu kwasababu ya kitu fulani, ni upendo wenye kutufanya kuwa watu wa kipekee sana tukiwa nao na tutakua watu watimilifu.

Kunamadhara makubwa sana kama hautakuwa na upendo huu wa kiMungu. Kwa maana kuna baadhi ya watu au watumishi wakishajiona wanuwezo wa kunena kwa lugha, wanombea na kutoa mapepo na unabii, na kusaidia watu wengine na kujiona wapo katika kiwango kizuri sana cha utakatifu lakini bila upendo huu wa kimungu ni sawa na bure. soma 1Wakorintho 13:2. Kwa maana upendo wa kimungu (AGAPE) ni upendo wa kiwango cha juu sana kuliko chochote, upendo usio isha.
tunasema upendo usio isha kawasabu, embu fikiria ukimpenda mtu kwa sababu ya kitu fulani. Je! siku akikosa hiko kitu bila shaka uo upendo utaisha. Lakini upendo wa Mungu wetu hauishi kwamaana anatupenda hadi hivi sasa hata tukimkosea na kumuudhi tukaomba toba yeye hutusamahe kwaajili ya upendo na kwakuwa tunakibali mbele zake.

Embu fikiria jinsi Mungu alivyoupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee (YESU), ili kila amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16
Tulikua wenye dhambi lakini kwa ajili ya upendo wa Mungu kutupenda sisi akaamua kumtoa mwanawe wa pekee ili tupate kuokolewa.

Mpendwa katika Bwana napenda nikutie nguvu katika hili, ukapate kua na upendo wa kimungu (AGAPE). Maana bila upendo huu ni sawa na bure.
waweza kujiuliza kwanini bila upendo huu ni sawa na bure ?

Soma biblia katika kitabu cha 1Wakorintho 13:1-3 na kuendelea kadri Mungu atakavyo zidi kukuongoza.
Hapo ndipo utaelewa ya kua bila upendo huu wa kipekee ambao Mungu anataka tuwe nao hakika utaingia katika kumchukiza yeye.
Kwamaana bila upendo huu utakua mtu wa kujisifia,kujiona wewe ndo bora kushinda wengine,kiburi kitainuka juu yako, lakini ukiwa na huu upendo hautakua navyo hivyo vyote kwamaana ukiwa na upendo huu hautajiona kuwa wewe ndio bora kuliko nk. Na ukiwa na upendo huu ambao Mungu hupendezwa nao hakika utaiponya nafsi yako na katika matendo yako yote utakayotenda katika kumuabudu Mungu hakika hayatakuwa sawasawa bure.

Hivyo basi kwa kulitambua hilo ni shauhuku ya moyo wangu ukapate kuwa na upendo wa hali ya juu sana, upendo wa kimungu maana kwa upendo huu utaweza kuishi maisha ya kitakatifu yenye utimilifu. Ikiwa itakuwia vigumu kua na upendo huu. Ningependa nikutie nguvu na uzidi kuomba ( Mathayo 7:7 ) ili ukapate kuishi ndani ya huu upendo wa kimungu na kufunga hila zote za shetani za kukufanya kushindwa kuwa na upendo huu ambao hata shetani mwenyewe hawezi kuuigilizia.

MUNGU NI PENDO NAYE APENDA WATU. TUWE NA UPENDO WAKE ILI TUSIWE SAWA NA BURE.

Jumanne, 15 Agosti 2017

MAMBO 3 YA KUKUSAIDIA UFANIKIWE KATIKA UFALME WA MUNGU.

LEO TUNAANGALIA JAMBO LA TATU


3. VIPAUMBELE SAHIHI

Kiwango cha mafanikio ya mtu kinategemea vipaumbele alivyo navyo. Kipaumbele cha kwanza tulichopewa na Mungu ni kuutafuta ufalme wake na haki yake na hayo yote tutazidishiwa (Matayo 6:33). Kipimo cha mafanikio ya mtu ni vipaumbele vyake. Maandiko yanasema tukiutafuta ufalme wa Mungu na haki yake uchumi mzuri, afya nzuri, furaha, amani nk tutazidishiwa.

Kwa hiyo kama tunavitafuta hivi vitu, maana yake hatuna vipaumbele sahihi mbele ya Mungu na tunaishi nje ya kusudi lake. Changamoto kubwa katika maisha ni kujua kitu gani cha kufanya. Lakini pia mafanikio yanategemea sana matumizi ya muda. Kama hujafanikiwa katika eneo fulani, tafuta majibu ya maswali yafuatayo:

a. Nini kusudi la Mungu kukuumba? (Mwanzo 1:26).
b. Nini maono ya Mungu juu yako? (Yeremia 1:5).
c. Nini vipaumbele vyako katika maisha yako? (Matayo 6:33).
d. Kwa nini unafanya hicho unachokifanya (nia ya kufanya unachofanya ni ipi)?
e. Je unatumiaje muda wako? (Waefeso 5:16).

Mungu anataka kukusaidia katika maisha yako kwa kutumia mpango wake. Maono ya Mungu juu ya maisha yako yatafanikishwa kwa mpango ambao Mungu ameuandaa. Mungu tayari alikuchagua hata kabla hujazaliwa (Waefeso 1:4—5). Hivyo Mungu alishaweka mpango wake juu ya maisha yako lakini wa kuamua kuishi kwa kiwango Mungu amekupangia siyo Mungu ila ni wewe.

PIA WAPENDWA TUZIDI KUA NA UPENDO KATIKA MAISHA YA UTAKATIFU.

MAMBO 3 YA KUKUSAIDIA UFANIKIWE KATIKA UFALME WA MUNGU.

LEO TUNAANGALIA JAMBO LA PILI

2. IMANI YA KUFANIKIWA:

Maandiko yanatuambia tunaishi kwa imani (Warumi 1:17). “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana” (Waebrania 11:1). Ukiunganisha Warumi 1:17 & Waebrania 11:1 utapata sentence inayosema: tunaishi kwa kuwa na uhakika na mambo yatarawajiwayo na bayana ya mambo yasiyoonekana.

Ili uweze kufanikiwa katika maisha yako, lazima uwe na uhakika kuwa unaenda kupata mafanikio. Tunafanikiwa kwa imani. Unapokuwa na uhakika wa kufanikiwa, utaweka bidii kuhakikisha unapata kile unachotegemea kupata. Kumbuka “imani pasipo matendo imekufa” (Yakobo 2:26).

Hivyo unapokuwa na uhakika wa mafanikio, na unafuata maelekezo ambayo Mungu anakupa, roho yako inafanikiwa. Na roho yako inapofanikiwa mafanikio yanaonekana katika maisha. Lakini pia kufeli kunahitaji imani. Mfano: kinachofanya watu wengi wawe wanafeli hesabu ni imani waliyoijenga katika hili som. Wengi wanaweka imani ya kutofanikiwa katika hesabu. Hivyo katika ulimwengu wa roho tayari wamefeli hata kabla ya kufanya mtihani. Ukiwa na imani ya kutofanikiwa hutakuwa na sababu ya kuweka juhudi ili ufanikiwe.

Unapojenga imani yako katika mafanikio, kuna sauti ya Mungu utaisikia itakayokupa uhakika wa kufanikiwa. Kumbuka imani chanzo chake ni kusikia (Warumi 10:17). Hivyo unapokuwa na uhakika wa kufanikiwa Mungu atakupa neno lililobeba mafanikio.

Lakini unapokuwa na imani ya kutofanikiwa, Shetani naye anakupa neno lililobeba kutofanikiwa. Hapa ndipo unasikia sauti kama “huwezi kufanikiwa katika biashara kwani hata wenzako hawajafanikiwa” au “huwezi kufaulu kwani hata wenye uwezo zaidi yako wamefeli.” Hizi ni sauti Shetani na unatakiwa uzikatae ndani yako kwa neno la Mungu. Mwambie Shetani kuwa mawazo ya Mungu juu yako ni mawazo ya mafanikio (Yeremia 29:11).

Hivyo jenga imani yako katika kufanikiwa. Maana yake kuwa na neno la Mungu ambalo limebaba mafanikio na liweke katika matendo. Unapomuomba Mungu kitu, yeye hutuma neno (Zaburi 107:20). Neno hili ndilo linakupa kusikia maelekezo ya Mungu juu ya kile anataka ufanye.

AMANI NA UPENDO VIKAPATE KUTAWALA NDANI YA MIOYONI MWETU

Jumatatu, 14 Agosti 2017

MAMBO 3 YA KUKUSAIDIA UFANIKIWE KATIKA UFALME WA MUNGU.

LEO TUNAANGALIA JAMBO LA 1

TAFSIRI YA CHANGAMOTO:

 Tunaishi katika ulimwengu wenye matatizo, changamoto, na majaribu mengi. Katika kila jaribu ambalo unakumbana nalo kuna mlango wa kutokea (1 Wakorintho 10:13).

Vikwazo au vipingamizi katika maisha wakati wote vipo lakini kufanikiwa au kutofanikiwa kunategemea na jinsi unavyotafsiri kile unachokutana nacho. Ukitafsiri changamoto za kimaisha kama kizuizi cha mafanikio, hakika hutafanikiwa lakini ukitafsiri kama fursa ya wewe kufanikiwa Mungu atakufanikisha (Hesabu 13 &14).

Yatazame matatizo kwa jicho la Mungu na siyo jicho la mwanadamu. Jicho la mwanadamu linaona dhambi na mauti lakini Mungu anaona msalaba na uzima wa milele. Hivyo katika kila changamoto jifunze kutafsiri kwa mtazamo wa kufanikiwa na siyo kutofanikiwa. Unapotafsiri kama fursa ya wewe kufanikiwa, akili yako itakupa njia za wewe kufanikiwa. Lakini unapotafsiri matatizo kama kipingamizi, akili yako itakupa sababu kwa nini hutofanikiwa.

Kiwango cha kufanikiwa kinategemea jinsi unavyoyatafsiri matatizo unayokutana nayo katika maisha. Unapoyatazama matatizo kama fursa ya wewe kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, unakuwa umemwambia Mungu kuwa “kwako hakuna kinachoshindikana.” Lakini unapotazama matatizo kama kizuizi cha wewe kuingia kanani unakuwa umemwambia Mungu “Mungu siamini kama unaweza kunifanikisha.”

Pia changamoto za maisha zisikufanye uwe unalalamika mbele za Bwana. Unapolalamika, Mungu anaweza kujibu kulalamika kwako bila kukujibu kile kinachokufanya ulalamike (Habakkuk 1—2).

Hivyo ijenge nafsi yako kuwa “nitafanikiwa” badala ya “sintafanikiwa.” Wakati wote, tafuta njia za kufanikiwa badala ya kuwaza kipi utafanya usipofanikiwa. Mafanikio yanaanzia ndani ndipo yanakuwa manifested kimwili. “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama roho yako ifanikiwavyo” (3 Yohana 1:2). Mtu wa nje ni matokeo ya yule mtu wa ndani.

Kwa hiyo katika maombi yako wakati wote nenda mbele za Bwana na fikra ya kufanikiwa. Kumbuka njia za Mungu siyo njia zetu (Isaya 55:8) na kwa Mungu yote yanawezekana (Matayo 19:26).


NENO LA LEO

NENO LA SIKU 

 *Msifadhaike mioyoni mwenu;* mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
YN. 14:1‭-‬3 SUV

 👉Mwaminini Mungu  tuu atatenda kwa mkono wake mwenyewe

👉Na kwa wakati wake
Acha kufadhaika

👉Acha kulia

👉Acha kukata tamaa

👉NI marufuku kukata tamaa kwa Mwana wa Mungu
👉Yeye ni Yule Jana. . Leo na hata milele
👉Amesema amekwenda kutuandalia makao
👉Naye atakuja kutuchukua

😒Usihofu kwa maana yeye ni baba wa wote
Atakufuta machozi

🚶🏻‍♀Yote unayopitia ni daraja tuu ya kukufikisha kwa Baba
🏃‍♀🏃‍♀Ongeza mwendo
Kama ulikuwa mmoja wapo wa waliochoka

👉Kuna wakati unasema unataka hata kujiua

👉Basi ni wakati wako wa kuamka na kusema
*
#SITAKUFA BALI
#NITAISHI NAMI #NIYASIMULIE #MATENDO #MAKUU YA #BWANA

🤔Usiruhusu kabisa mawazo hayo
👯👯‍♂Simama tena tukapaone alipotuandalia Baba yetu panavyofanana mfano wake unaambiwa hakuna hapa duniani.

😊🤗Haleluyaaaaa🙌🙌

👉Basi Ujumbe wako huo

Jumapili, 13 Agosti 2017

JINSI YA KUANDIKA MAJINA KIUTAKATIFU

​Tumsifu YESU KRISTO​  Tujifunze jinsi ya kuandika haya majina na utofauti wake,
  1.  ukiandika
          mungu
soma 2korintho 4:4
soma 2wafalme 1:2
       kumbe hapo inamaana shetani
2.  ukiandika
      Mungu au
     MUNGU
soma Yohana 3:16
soma Luka 1:26
     hapo inamaana Muumba mbingu na nchi
3.  ukiandika
    bwana
soma Mathayo 25:5
    kumbe ukiandika herufi ndogo inamaana bwana mume, au bos wako wa kazi
4.  ukiandika
       Bwana au
        BWANA
soma Mathayo 22:37
   hapo ni Mungu mwenyewe
5.  ukiandika
      roho
soma Luka 9:56
hapo maana yake roho yako roho za mashetani
6.  ukiandika
    Roho au
     ROHO
soma Yohana 14:26
  hapo ni Mungu mwenyewe
7.  ukiandika
      yesu
hapo ni bar yesu
  mchawi yule
       matendo 13:6
8.  ukiandika
        Yesu au
        YESU
soma Mathayo 1:16
hivyo kua makini na uandishi wa majina haya barikiwa na Bwana

Ijumaa, 11 Agosti 2017

WOKOVU KATIKA AGANO JIPYA.

SHALOM MPENDWA KATIKA BWANA. Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP "UW"  Leo tunaenda kujifunza kuhusu wokovu. ...