Jumanne, 15 Agosti 2017

MAMBO 3 YA KUKUSAIDIA UFANIKIWE KATIKA UFALME WA MUNGU.

LEO TUNAANGALIA JAMBO LA PILI

2. IMANI YA KUFANIKIWA:

Maandiko yanatuambia tunaishi kwa imani (Warumi 1:17). “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana” (Waebrania 11:1). Ukiunganisha Warumi 1:17 & Waebrania 11:1 utapata sentence inayosema: tunaishi kwa kuwa na uhakika na mambo yatarawajiwayo na bayana ya mambo yasiyoonekana.

Ili uweze kufanikiwa katika maisha yako, lazima uwe na uhakika kuwa unaenda kupata mafanikio. Tunafanikiwa kwa imani. Unapokuwa na uhakika wa kufanikiwa, utaweka bidii kuhakikisha unapata kile unachotegemea kupata. Kumbuka “imani pasipo matendo imekufa” (Yakobo 2:26).

Hivyo unapokuwa na uhakika wa mafanikio, na unafuata maelekezo ambayo Mungu anakupa, roho yako inafanikiwa. Na roho yako inapofanikiwa mafanikio yanaonekana katika maisha. Lakini pia kufeli kunahitaji imani. Mfano: kinachofanya watu wengi wawe wanafeli hesabu ni imani waliyoijenga katika hili som. Wengi wanaweka imani ya kutofanikiwa katika hesabu. Hivyo katika ulimwengu wa roho tayari wamefeli hata kabla ya kufanya mtihani. Ukiwa na imani ya kutofanikiwa hutakuwa na sababu ya kuweka juhudi ili ufanikiwe.

Unapojenga imani yako katika mafanikio, kuna sauti ya Mungu utaisikia itakayokupa uhakika wa kufanikiwa. Kumbuka imani chanzo chake ni kusikia (Warumi 10:17). Hivyo unapokuwa na uhakika wa kufanikiwa Mungu atakupa neno lililobeba mafanikio.

Lakini unapokuwa na imani ya kutofanikiwa, Shetani naye anakupa neno lililobeba kutofanikiwa. Hapa ndipo unasikia sauti kama “huwezi kufanikiwa katika biashara kwani hata wenzako hawajafanikiwa” au “huwezi kufaulu kwani hata wenye uwezo zaidi yako wamefeli.” Hizi ni sauti Shetani na unatakiwa uzikatae ndani yako kwa neno la Mungu. Mwambie Shetani kuwa mawazo ya Mungu juu yako ni mawazo ya mafanikio (Yeremia 29:11).

Hivyo jenga imani yako katika kufanikiwa. Maana yake kuwa na neno la Mungu ambalo limebaba mafanikio na liweke katika matendo. Unapomuomba Mungu kitu, yeye hutuma neno (Zaburi 107:20). Neno hili ndilo linakupa kusikia maelekezo ya Mungu juu ya kile anataka ufanye.

AMANI NA UPENDO VIKAPATE KUTAWALA NDANI YA MIOYONI MWETU

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

WOKOVU KATIKA AGANO JIPYA.

SHALOM MPENDWA KATIKA BWANA. Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP "UW"  Leo tunaenda kujifunza kuhusu wokovu. ...