SHALOM MPENDWA KATIKA BWANA.
Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP "UW"
Leo tunaenda kujifunza kuhusu wokovu.
Ukisoma Biblia yako katika kitabu cha Efeso 2:8 inasema " nanyi mmeokolewa kwa neema kwa njia ya imani." yaani tumepata kuokolewa (WOKOVU) kwa NEEMA kwa njia ya IMANI. Hayo ndiyo maneno ya agano jipya yenye kumtukuza Yesu. Ya kwamba ndiye aliyetimiza hayo.
WOKOVU halisi ndio aliouleta Yesus Kristo, yeye ndiye aliyeleta wokovu hapa duniani, na wala hapana mwingine aliyeleta wokovu kama huu. Yesu alikuja kutukomboa kutoka dhambini.
1Petro 2:24 " yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki;na kwakupigwa kwake mliponywa."
Shida kubwa ya watu wengi hawataki kumwamini Yesu, na hata wale ambao wamekwisha mwamini bado wanajiona ni wenye dhambi, na bado wengi wao wanateswa na dhambi, bado shetani anaendelea kuyashikilia maisha yao, leo hii nina habari njema juu yako ya kuwa, ukishaokolewa unasamehewa dhambi na Mungu hatazikumbuka tena hizo dhambi zako. Nawe utapata kuishi kwa ile neema ya Mungu, na hata ikatokea ukaanguka dhambini bado neema ya kukuokoa kutoka dhambini, na hakika utaokolewa na Mungu atakusamehe kabisa.
Waebrania 8:12 " kwasababu nitawasamehe maovu yao, na dhambi zao sitazikumbuka tena"
Leo hii shetani amekamata fikra za wapendwa wengi sana, na kuwakumbusha dhambi zao, na kujiona si kitu machoni pa Bwana, kwakua shetani anawakumbusha dhambi ili wajione ni wenye dhambi, nataka nikwambie kitu, Mungu akishasamehe dhambi zako, azikumbuki tena, na anakupa neema ya kukusamehe na kukuokoa pindi uingiapo kwenye majaribu. Usijione tena mwenye dhambi ndani ya Kristo Yesu, jihesabie mwenye haki, na mwenye neema ile ya kukukomboa kutoka dhambini ili shetani asiishike nafsi yako na kijiona huna kitu machoni pa Bwana maana shetani anakamata fikra za watu ili apate kuwatenganisha mbali na imani ya Yesu Kristo.
Soma Biblia katika kitabu cha Mathayo 11:28 " njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Soma Biblia katika kitabu cha Zaburi 68:12 "Na ahimidiwe Bwana, siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu"
Mpendwa katika Bwana Mungu wetu ndiye mwokovu wetu anayetuokoa na kututua mizigo yetu siku hadi siku, naye anasema twendeni kwake wenye kuelemewa na mizigo naye atatupumzisha, unaweza ukawa unafanya dhambi bila wewe kufahamu, lakini po neema, kadri unavyozidi kumtumainia Mungu, dhambi zinajiachia kila siku, kwamaana hututua mizigo yetu siku kwa siku.
Mungu wetu hajatukomboa tu na dhambi bali alitukomboa na dunia hii mbovu
Wagalatia 1:4 " ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu"
Hii dunia tunayoishi, ni dunia mbovu yenye kujaa kila aina ya kazi za ibilisi ambaye anafanya kila aina ya njama ili kututenga mbali na Mungu wetu.Ashukuriwe Yesu ametuokoa na kazi mbovu hizi za ibilisi, kwa maana sisi hatukupokea roho ya dunia kwamaana ni mbovu, mija ya kazi za ibilisi ni "kiburi".
Nataka nikwambie kitu mpendwa, kama unasumbuliwa na mizigo ya dhambi, kama unasumbuliwa na kazi mbovu za mwovu ibilisi, wewe uliyejiona si kitu machoni pa bwana kumbuka ipo neema juu yako, ipo neema kwa Yesu Kristo, yeye aliyesema njoeni nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzinsha, yeye atuondoleaye mizigo siku hadi siku, hakika ni muweza wa yote kwake aaminiye. Ukimtumainia naye atafanya makubwa katika maisha yako na shetani hatapata nafasi tena.
Mtumishi wa Yesu
@Henry Sebastian Kibanga
Kipaombele > Mathayo 6:33
FB page: UPENDO WORSHIP
INSTAGRAM: UPENDO WORSHIP
http://upendoworship.blogsport.co.id/?m=1
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
WOKOVU KATIKA AGANO JIPYA.
SHALOM MPENDWA KATIKA BWANA. Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP "UW" Leo tunaenda kujifunza kuhusu wokovu. ...
-
SHALOOM Mpendwa katika BWANA. Karibu tena katika kujifunza neno la Mungu katika blog yako pendwa UpendoWorship Leo tunaenda kujifu...
-
SHALOOM. Mpendwa katika BWANA Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP Tukapate kujifunza sala mbali mbali za kutukomboa kuto...
-
LEO TUNAANGALIA JAMBO LA PILI 2. IMANI YA KUFANIKIWA : Maandiko yanatuambia tunaishi kwa imani (Warumi 1:17). “Basi imani ni kuwa na ha...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni