Jumamosi, 16 Septemba 2017

MAMBO YANAYOTOKEA BAADA YA KUOKOKA

SHALOM WAPENDWA KATIKA BWANA

Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP

Leo tunaenda kujifunza mambo kadhaa ambayo yanatokea baada ya mtu kuokoka ( kumkubali YESU kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yake)

Amini nakwambia kuna mambo mengi sana yanatokea katika ulimwengu wa Roho pindi mtu anapoamua kumpokea YESU KRISTO kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yake. Baadhi ya mambo hayo ni;

1: UNAKUA KIUMBE KIPYA

Ukisoma 2Korintho 5:17 "hata imekua mtu akiwa ndani ya Kristo amekua kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama yamekuwa mapya." Yaani unakua umezaliwa mara ya pili, kuzaliwa mara ya pili ni kile kitendo cha mtu kubadilisha maisha yako ya kale kabla ya kumpokea YESU, ila pale tu mtu unapompokea Yesu ndipo unakua umezaliwa mara ya pili.

2: KUINGIA KATIKA UFALME WA MBINGUNI

Yesu akajibu, akamwambia Amin, amin nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa mbinguni. " Yohana 3:3" 
Kwaio tunaona bila ya kuwa kiumbe kipya, bila ya kuzaliwa mara ya pili huwezi kuuona ufalme wa mbinguni. Na ufalme wa mbinguni ndiko kwenye kila kitu na ndiko Mungu anataka tuishi katika ufalme huo wa mbinguni. 
Mathayo 6:33 "Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo yote mtazidishiwa.
Hivyo basi unaona ni jinsi gani ilivyo muhimu mtu kuzaliwa mara ya pili ( kumpokea Yesu Kristo) maana ndipo penye kukupeleka katika Ufalme Wa Mbinguni.

3: UNAKUA MWENYE BARAKA.

Ukisome kisoma kwenye Biblia Waefeso 1:3 inasema " Atukuzwe Mungu, baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo.
Hakika utakuwa mbarikiwa kwa baraka zote za rohoni katika Kristo Yesu.

4: UNAKUA SIO MTUMWA TENA WA MAOVU (DHAMBI), UNAKUA HURU

Ukiwa kiumbe kipya, ukaingia katika ufalme wa mbinguni na kuwa mwenye baraka, Kumbuka Yesu alikufa pale msalabani kwaajili ya dhambi zetu, ile damu iliyomwagika pale msalabani ilitukomboa kutoka kwa yule mwovu shetani, kwa maana huko ndiko kwenye dhambi na kila aina ya uovu, sasa uwezi kuushinda huo uovu kama hujaamua kumkabidhi Yesu maisha yako, hivyo unapoamua kuokoka unakua unaingizwa katika ufalme wake Mungu.
Ukisoma katika Biblia kitabu cha Wakolosai 1:13-14 "Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake, ambayo katika yeye tunaukombozi, yaani masamaha wa dhambi.

Hivyo ukiokoka huru, mwenye kusamehewa dhambi zako zote, na unakua sio mtumwa tena wa dhambi, maana atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi, na mshahara wa dhambi ni mauti.
 " Warumi 6:23"

5: KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU

Unapoamua kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako na kumtumainia yeye, ukimwomba atakupatia Roho mtakatifu ndani yako kwa ajili ya kukuongoza katika maisha yako. Yesu hutubatizwa kwa Roho mtakatifu " Marhayo 3:11 " na ndio ubatizo wenye thamani kubwa sana kwa maana unashuhudia mbinguni na duniani.

Roho Mtakatifu atakuongoza katika
-Maisha yako
-Kukufundisha neno la Mungu
-Hukumbusha neno la Mungu
-Kukufunua akili zako na kuyaelewa maandiko
Kuna mengi sana ambayo Roho mtakatifu atkuongoza ili ukapate kuishi maisha ya kiutakatifu katika ufalme wa mbinguni

Kwakusema hayo, yapo mengi tu amayo hutokea katika ulimwengu wa kiroho pale mtu akiamua kuokoka, mtummoja akiokoka ni shangwe na furaha tupu Mbingun,
Hivyo katika maisha haya hakuna uamuzi mzuri na mkubwa kushunda yote kama mtu anapoamua kumkabidhi Yesu maisha yake, kama kweli unataka kumuona Mungu katika maisha yako. Mkabidhi Yesu maisha yako.


Mtumishi wa Yesu
@Henry Sebastian Kibanga
Kipaombele > Mathayo 6:33
FB: UPENDO WORSHIP
IG: UPENDO WORSHIP
http://upendowotship.blogspot.co.id/?m=1

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

WOKOVU KATIKA AGANO JIPYA.

SHALOM MPENDWA KATIKA BWANA. Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP "UW"  Leo tunaenda kujifunza kuhusu wokovu. ...