Jumapili, 20 Agosti 2017

UADUI KATI YA MWANAMKE NA SHETANI.1

SHALOOM Mpendwa katika BWANA.

Karibu tena katika kujifunza neno la Mungu katika blog yako pendwa UpendoWorship


Leo tunaenda kujifunza juu ya uadui uliopo kati ya mwanamke na mwovu shetani.

Labda nianze na kukuuliza swali ambalo nilikua najiuliza hapo kabla, kwanini katika mikutano ya injili, semina mbalimbali za maombezi, na makanisani pia, idadi kubwa sana ya watu wanaosumbuliwa na shetani (mapepo) ni wanawake. Sio kwamba wanaume hawasumbuliwi na mapepo, lakini hapa naangalia idadi kubwa ambayo ni wanawake.
Je! Ulishawahi jiuliza ni kwanini? Bila shaka kwa akili za kibinadamu ni vigumu kutambua hilo, lakini bila shaka, kwa kile chochote kinachoendelea duniani hakika kilishawahi kuandikwa kwenye biblia. Je! maandiko yanasema nini juu ya hili

Ukisoma kwenye kitabu cha biblia Mwanzo 3:13-15 inasema

Mwanzo 3:13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.
Mwanzo 3:14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;
Mwanzo 3:15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. 

Nyoka anayezungumziwa hapo ni shetani, hivyo basi ukiangalia mstari wa 15 apo ndipo utaona kabisa ya kwamba Mungu aliweka uadui kati ya mwanamke na yule nyoka(shetani). Hivyo basi kwa uzao wa mwanamke atamponda kichwa nyoka, naye nyoka atakuponda kisigino ewe mwanamke. Tufaham ya kuwa uzao wa mwanamke ni wale watoto ambao atakuja kuzaa (mimI na wewe tu uzao wa mwanamke) na uzao wa shetani ni mapepo.

Mpaka kufikia hapo nafkiri ushaanza kupata picha halisi ya kua uadui huu umeanzia wapi, na ni kwanini idadi kubwa wanaoteswa na shetani(mapepo) ni wanawake, hii yote ni kwasabu Mungu alishaweka uadui kati yao. Unaweza ukawa unajiuliza kwanini aliweka uadui. Jibu ni kwamba

Ukisoma Biblia kitabu cha Mwanzo 1:1-6, Hapo ndipo utaona ya kua kwanini Mungu alieka uadui kati ya hawa wawili, kwa maana nyoka alimdanganya mwanamke, akala lile tunda kwa kumwambia hatakufa bali atajua mema na mabaya angali walikatazwa na Mungu wasije kula tunda la mti huo.
Mungu alichukizwa na hiko kitendo kiasi akaweka uadui kati yao.

Baada ya kulifahamu hilo, chimbuko la uadui huo twende moja kwa moja katika biblia kitabu cha Ufunuo 12:1-11 na kuendelea mpaka mstari wa 17 ( Ufunuo 12:1-17)

Ni shauku ya moyo wangu upate kusoma hapo li upate maana halisi ya uadui huo na jinsi ulivyokua ukiendelea.

Ukisoma hapo utapata kuona kuna ishara kuu iliyoonekana kutoka Mbinguni, Mwanamke mwenye mimba akilia kwa utungu na kuumwa katika kuzaa, ikaonekana ishara nyingine na tazama joka kubwa(shetani) na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni( nyota hizo ni mapepo) na kuziangusha katika nchi, pia na yule joka akasimama kwa yule mwanamke ili azaapo amle yule mtoto wake. Naye yule mwanamke akazaa mtoto mwanamume naye atakayechunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu na kiti cha enzi. Je mtoto huyo ni nani? Jibu ni Yesu Kristo. Hapo ndipo likatimia lile andiko lisemalo kwa uzao wako ewe mwanamke utamponda kichwa nyoka(shetani). Yesu alimponda kichwa shetani pale msalabani.

Ukisoma Ufunuo 12:15 utazidi kuona ule uadui jinsi unavyozidi, kwa maana nyoka akazidi kupambana na mwanamke, nyoka akatoa katika kinywa chake nyuma ya huyo mwanamke maji kama mto, ili amfanye kuchukuliwa na mto huo yule mwanamke, mstari wa 16 unatuambia Nchi(ardhi) ikamsaidia mwanamke, Nchi ikaifunika kinywa chake,ikaumeza mto ule alioutoa yule nyoka.

(Nyoka anapambana na mwanamke lakini pia nchi"ardhi" inamsaidia mwanamke na ndomana moja ya vita kuu ya kiroho ipo kwenye ardhi, kwasababu pia ardhi ilimsaidia mwanamke)

mstari wa 17, chuki ikazidi kwa maana yule nyoka(shetani) akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake akafanye vita juu ya wazao wake waliosalia(wazao wake hao ni mimi na wewe) wazishikao amri za Mungu, na kua na ushuhuda wa Yesu.....

Natumaini mpaka kufikia hapo ushapata picha halisi kwanini shetani anapambana sana na mwanamke kwa njia mbalimbali iwe kuharibu mimba,kumpandikizia magonjwa,mapepo,mateso, kumfanya mwanamke kutojitambua na kuishi maisha ya kianasa kama ilivyo hivi sasa,hii yote kwasababu ya ule uadui kwa maana shetani anapiagana na hii vita ili kuwinda kile kilichopo ndani ya mwanamke ili kisije kumponda kichwa. Naye shetani akisha kufanikisha kwa kuharibu kwa mwanamke apo tunasema nyoka amekuponda kisigino.

Yesu alipokuja alipitia kwa mwanamke(kwa uweza wa Roho mtakatifu). Likatimia neno, kwa uzao wa mwanamke shetani atapondwa kichwa.

Ewe mwanamke kumbuka vita hii si juu ya damu na nyama bali ni vita ya kiroho, hivyo tambua Mungu ameweka kitu cha pekee kabisa kupitia kwako, hivyo usiishi kizembe zembe, kila mara kumbuka kuombea uzao wako,ombea familia yako ijayo(kama bado huna mtoto), kila mara ombea ardhi,ombea akili yako isije kamatwa na mwovu,ombea fahamu zako, usihishi kibahati mbaya, wewe ni mtu wa tofauti kabisa,usikubali nyoka(shetani) akuponde kwenye kisigino,ombea watoto wako, usiruhu mateso ya kimapepo(uzao wa shetani) yakutese maishni mwako,ombea kila kitu kinachoitwa kwa jina lako, (naposema ombea kila kitu kinachoitwa kwa jina lako namaanisha hata mchumba uliye naye au maraiki au mumeo kwa maana shetani pia anaweza akawatumia hao hao kuja kukuharibia uzao wako)

 Kumbuka tunaye Yesu muweza wa yote, hakuna ashindwalo, kwake yeye utapata kumponda kichwa shetani kama yeye alivyomponda pale msalabani.

usisahau ku share ili pia na wenzako wapate kushiriki baraka za ibada hii
@Henry Sebastian Kibanga.
Instagram@UPENDO WORSHIP

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

WOKOVU KATIKA AGANO JIPYA.

SHALOM MPENDWA KATIKA BWANA. Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP "UW"  Leo tunaenda kujifunza kuhusu wokovu. ...