Alhamisi, 17 Agosti 2017

UPENDO WENYE KUZIPONYA NAFSI ZETU

JIFUNZE KUWA NA UPENDO WA KIMUNGU.

Yawezekana kabisa ukawa unafahamu nini maana ya upendo. Labda kwa kusema hivi,
Upendo ni jinsi vile mtu apendavyo iwe kihisia au kutamania au kuweka kitu au jambo kuwa kipaombele ndio kupenda. Wengine husema upendo ni ile hali ya kuwa na amani moyoni juu ya kitu fulani.
Inawezekana ikawa ivyo lakini ni kwa njia ya kila mtu na kwa jinsi alivyopokea neno upendo.
lakini kuna vyanzo vingi sana vya upendo, nazungumzia vitu ambavyo vinamfanya mtu kupelekea kupenda.

Kuna upendo wa kumpenda mtu kwa sababu ya kitu fulani alicho nacho kwa dhumuni la kusaidiwa au kutimiza haja zako.

Kuna upendo wa kindugu, huu ni ule upendo mtu anampenda nduguye, yupo radhi kwenda kulala nae kitanda kimoja hospitali kwa ajili ya kumuhudumia. ( chanzo ni ndugu, lakini asingekua ndugu yake au rafiki yake asingempenda)

Kuna upendo huwa unaibuka kwasababu tu jinsi mtu anaevyoendesha shughuli zake za kimaisha kutokea kupenda vitu kadha wa kadha. (vyanzo maranyingi huwa ni tamaa,ushawishi nk.)

Ukiangalia kwa makini kuna jinsi nyingi sana watu hupelekea kuwa na upendo juu ya kitu au mtu fulani katika maisha yao. Pia inafikia mahala uo upendo walio nao waweza kupelekea kuharibikiwa kimaisha kwa sababu mbali mbali.
Je ni kwanini upendo huo hupelekea kuharibikiwa au kupata matatizo katika maisha yao. Naweza sema ni kwasababu unakua si upendo ambao Mungu wetu mkuu ametuagiza tuwe nao katika maisha yetu.
Mfano upendo ambao Mungu hajaagiza ni kumpenda mtu kwasababu ya kitu fulani, hii itakupelekea kumtegemea mtu huyo kwa ajili ya shida zako. Na pindi unapomtegemea mtu kumbuka Mungu alisema nini katika kitabu cha Yeremia 17:5.

Je Upendo wa Kweli Ni upi ? Upendo aliotuagiza Mungu tuwe nao ni upi ? Au Mungu wetu ana upendo upi ? ili tuufate upendo wa Mungu wetu.

Ukisoma Yohana 3:16 utapata kuuona upendo ambao Mungu wetu anao.
Upendo wa Agape . Huu ni upendo ambao Mungu ametuagiza (anapenda) tuwe nao, ni ule upendo wa hali ya juu sana, ni upendo ambao Mungu wetu mwenyewe anao,upendo ambao haujivuni, upendo ambao hautampenda mtu tu kwasababu ya kitu fulani, ni upendo wenye kutufanya kuwa watu wa kipekee sana tukiwa nao na tutakua watu watimilifu.

Kunamadhara makubwa sana kama hautakuwa na upendo huu wa kiMungu. Kwa maana kuna baadhi ya watu au watumishi wakishajiona wanuwezo wa kunena kwa lugha, wanombea na kutoa mapepo na unabii, na kusaidia watu wengine na kujiona wapo katika kiwango kizuri sana cha utakatifu lakini bila upendo huu wa kimungu ni sawa na bure. soma 1Wakorintho 13:2. Kwa maana upendo wa kimungu (AGAPE) ni upendo wa kiwango cha juu sana kuliko chochote, upendo usio isha.
tunasema upendo usio isha kawasabu, embu fikiria ukimpenda mtu kwa sababu ya kitu fulani. Je! siku akikosa hiko kitu bila shaka uo upendo utaisha. Lakini upendo wa Mungu wetu hauishi kwamaana anatupenda hadi hivi sasa hata tukimkosea na kumuudhi tukaomba toba yeye hutusamahe kwaajili ya upendo na kwakuwa tunakibali mbele zake.

Embu fikiria jinsi Mungu alivyoupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee (YESU), ili kila amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16
Tulikua wenye dhambi lakini kwa ajili ya upendo wa Mungu kutupenda sisi akaamua kumtoa mwanawe wa pekee ili tupate kuokolewa.

Mpendwa katika Bwana napenda nikutie nguvu katika hili, ukapate kua na upendo wa kimungu (AGAPE). Maana bila upendo huu ni sawa na bure.
waweza kujiuliza kwanini bila upendo huu ni sawa na bure ?

Soma biblia katika kitabu cha 1Wakorintho 13:1-3 na kuendelea kadri Mungu atakavyo zidi kukuongoza.
Hapo ndipo utaelewa ya kua bila upendo huu wa kipekee ambao Mungu anataka tuwe nao hakika utaingia katika kumchukiza yeye.
Kwamaana bila upendo huu utakua mtu wa kujisifia,kujiona wewe ndo bora kushinda wengine,kiburi kitainuka juu yako, lakini ukiwa na huu upendo hautakua navyo hivyo vyote kwamaana ukiwa na upendo huu hautajiona kuwa wewe ndio bora kuliko nk. Na ukiwa na upendo huu ambao Mungu hupendezwa nao hakika utaiponya nafsi yako na katika matendo yako yote utakayotenda katika kumuabudu Mungu hakika hayatakuwa sawasawa bure.

Hivyo basi kwa kulitambua hilo ni shauhuku ya moyo wangu ukapate kuwa na upendo wa hali ya juu sana, upendo wa kimungu maana kwa upendo huu utaweza kuishi maisha ya kitakatifu yenye utimilifu. Ikiwa itakuwia vigumu kua na upendo huu. Ningependa nikutie nguvu na uzidi kuomba ( Mathayo 7:7 ) ili ukapate kuishi ndani ya huu upendo wa kimungu na kufunga hila zote za shetani za kukufanya kushindwa kuwa na upendo huu ambao hata shetani mwenyewe hawezi kuuigilizia.

MUNGU NI PENDO NAYE APENDA WATU. TUWE NA UPENDO WAKE ILI TUSIWE SAWA NA BURE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

WOKOVU KATIKA AGANO JIPYA.

SHALOM MPENDWA KATIKA BWANA. Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP "UW"  Leo tunaenda kujifunza kuhusu wokovu. ...