Jumatatu, 4 Septemba 2017

KUFANYA IBADA KIUTAKATIFU

MAMBO MUHIMU KATIKA KUIFANYA IBADA KIUTAKATIFU

1.MOYO (ROHO)

Moyo unanafasi kubwa sana katika kukamilisha ibada kiutakatifu. Kwamaana moyoni ndiko kutokako mawazo, ndiko kwenye mawasiliano na Mungu, hivyo usipouandaa moyo wako kwa kupokea neno, kusikiliza neno, kuruhusu au kuamini uweza wa Kimungu hakika hutapokea wala kuifanya ibada kiutakatifu. Kwakusema hayo inatupasa kuiandaa mioyo yetu kuwa safi kabisa kwa maana tutamuona Mungu

"Mathayo 5:8" (HERI WENYE MOYO SAFI KWA MAANA WATAMUONA MUNGU)

usipokua na Moyo safi usitegemee kumuona Mungu kwa namna yoyote ile.

Usiwe na moyo (Roho) wa kusita sita, usiingize hofu, wala usiiache imani yako kukaa mbali na moyo (Roho) waako katika kufanya ibada.

Embu fikiria yule mwanamke aliye gusa pindo la Yesu, tazama jinsi alivyouandaa moyo wake kiimani, aliuandaa moyo kiukamilifu kabisa naye alipogusa pindo akapokea uponyaji.
Nasi leo hii tukitaka kupokea miujiza ya Mungu wetu ni lazima kuiandaa mioyo yetu kiukamilifu ili tupate kupokea katika kufanya kwetu ibada.

 2.KUSIFU NA KUABUDU

Hakika Mungu wetu huketi katika sifa, kadri unavyo msifu na kumuabudu ndivyo anavyozidi kujitukuza katika maisha yako. Mnyenyekeeni Mungu, mwabuduni yeye na kulitukuza jinalake. Kwa kusifu na kuabudu katika Roho na kweli ROHO WA MUNGU HUWAALIKA MALAIKA WATAKATIFU KUFANYA KITUO KATI YA MOYO WAKO NA MBINGUNI.

Tazama Paulo na Sila walivyofungwa gerezani, kwajinsi walivyokuwa wakimuamini Mungu (kutoka moyoni mwao) wakaanza kuomba na kumwimbia Mungu nyimbo za kusifu na tazama milango ya gereza ikafunguka. "Matendo ya Mitume 16:25-26"

Tazama jinsi walivyo sifu, Mungu alishuka kati yao kwa maana Mungu wetu huketi katika sifa.
Leo hii watu huona kumsifu Mungu ni kama kitu cha kawaida, kwamfano waimbaji kanisani wanapo sifu, watu huona ni kawaida, watu wanakaa chini (kwenye viti) yaani kanakwamba walilazimishwa kufanya ibada au kwenda kanisani, kwakufanya hivyo usitegemee Mungu ashuke kati yako kama humsifu, hakika kama na wewe ni mmoja wapo hacha kabisa io tabia, inaonyesha ni jinsi gani hata moyoni haupo safi kwamaana laiti ungalitambua toka moyoni uweza wa Mungu wetu mkuu, ungalisimama na kumsifu Mungu ili kuifanya ibada yako kuwa takatifu na kuruhusu Mungu ashuke na kufanya mapenzi yake.

Hakika msifuni Bwana kwa maana fadhili zake ni za milele.

 3.SADAKA

Sadaka ni kitu kimoja cha muhimu sana katika kushiriki ibada kitakatifu, ni ibada iliyo kamilika. Ibada hukamilishwa kwa kumtolea Mungu sadaka, sadaka ni mbegu iliyo bora, hata neno la Mungu lasema nijaribuni kwa matoleo yenu. Matoleo ndio sadaka, unavyomtolea Mungu kile ulicho nacho kwamaana kadri Mungu atakavyo kuongoza hakika unakua unafanya ibada kikamilifu. Tunasema kadri Mungu atakavyo kuongoza tukimaanisha usitoe sadaka kimazoea.  Toa Sadaka kadri Mungu atakavyo kuongoza. Mungu hupendezwa na sadaka umtoleayo.

Embu fikiria Mtu anaishi maisha ya gharama sana lakini akienda kanisani kwavile amezoea kutoa sadaka sh.500 basi kila siku ni hiyo hiyo hakika hutaweza kufanya ibada kamilifu yenye kumpendeza Mungu. Toa sadaka kadri Mungu atakavyo kushuhudia moyoni mwako ili ikapate kumpendeza Mungu wetu.


UPENDO WORSHIP
http://upendoworship.blogspot.co.id/?m=1
servant of Jesus
@Henry Sebastia Kibanga

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

WOKOVU KATIKA AGANO JIPYA.

SHALOM MPENDWA KATIKA BWANA. Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP "UW"  Leo tunaenda kujifunza kuhusu wokovu. ...