LEO TUNAANGALIA JAMBO LA 1
TAFSIRI YA CHANGAMOTO:
Tunaishi katika ulimwengu wenye matatizo, changamoto, na majaribu mengi. Katika kila jaribu ambalo unakumbana nalo kuna mlango wa kutokea (1 Wakorintho 10:13).
Vikwazo au vipingamizi katika maisha wakati wote vipo lakini kufanikiwa au kutofanikiwa kunategemea na jinsi unavyotafsiri kile unachokutana nacho. Ukitafsiri changamoto za kimaisha kama kizuizi cha mafanikio, hakika hutafanikiwa lakini ukitafsiri kama fursa ya wewe kufanikiwa Mungu atakufanikisha (Hesabu 13 &14).
Yatazame matatizo kwa jicho la Mungu na siyo jicho la mwanadamu. Jicho la mwanadamu linaona dhambi na mauti lakini Mungu anaona msalaba na uzima wa milele. Hivyo katika kila changamoto jifunze kutafsiri kwa mtazamo wa kufanikiwa na siyo kutofanikiwa. Unapotafsiri kama fursa ya wewe kufanikiwa, akili yako itakupa njia za wewe kufanikiwa. Lakini unapotafsiri matatizo kama kipingamizi, akili yako itakupa sababu kwa nini hutofanikiwa.
Kiwango cha kufanikiwa kinategemea jinsi unavyoyatafsiri matatizo unayokutana nayo katika maisha. Unapoyatazama matatizo kama fursa ya wewe kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, unakuwa umemwambia Mungu kuwa “kwako hakuna kinachoshindikana.” Lakini unapotazama matatizo kama kizuizi cha wewe kuingia kanani unakuwa umemwambia Mungu “Mungu siamini kama unaweza kunifanikisha.”
Pia changamoto za maisha zisikufanye uwe unalalamika mbele za Bwana. Unapolalamika, Mungu anaweza kujibu kulalamika kwako bila kukujibu kile kinachokufanya ulalamike (Habakkuk 1—2).
Hivyo ijenge nafsi yako kuwa “nitafanikiwa” badala ya “sintafanikiwa.” Wakati wote, tafuta njia za kufanikiwa badala ya kuwaza kipi utafanya usipofanikiwa. Mafanikio yanaanzia ndani ndipo yanakuwa manifested kimwili. “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama roho yako ifanikiwavyo” (3 Yohana 1:2). Mtu wa nje ni matokeo ya yule mtu wa ndani.
Kwa hiyo katika maombi yako wakati wote nenda mbele za Bwana na fikra ya kufanikiwa. Kumbuka njia za Mungu siyo njia zetu (Isaya 55:8) na kwa Mungu yote yanawezekana (Matayo 19:26).
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
WOKOVU KATIKA AGANO JIPYA.
SHALOM MPENDWA KATIKA BWANA. Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP "UW" Leo tunaenda kujifunza kuhusu wokovu. ...
-
SHALOOM Mpendwa katika BWANA. Karibu tena katika kujifunza neno la Mungu katika blog yako pendwa UpendoWorship Leo tunaenda kujifu...
-
SHALOOM. Mpendwa katika BWANA Karibu tena katika blog yako pendwa ya UPENDO WORSHIP Tukapate kujifunza sala mbali mbali za kutukomboa kuto...
-
LEO TUNAANGALIA JAMBO LA PILI 2. IMANI YA KUFANIKIWA : Maandiko yanatuambia tunaishi kwa imani (Warumi 1:17). “Basi imani ni kuwa na ha...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni